Home News Inspekta Generali Joseph Boinett apongeza wakaazi wa Pokot Magharibi na Turkana kwa kudumisha amani

Inspekta Generali Joseph Boinett apongeza wakaazi wa Pokot Magharibi na Turkana kwa kudumisha amani

1 min read
0
0
img_20161227_092904.jpg
Share This

​Inspekta generali wa polisi Joseph Boinett, Jumatatu alijumuika na viongozi wa Pokot Magharibi na Turkana pamoja na wenyeji katika sherehe za siku ya krismasi sehemu ya Tukwel.

Madhumuni makuu ya mjumuiko huo ikiwa ni kuwashukuru wenyeji kwa kudumisha amani kwa muda mrefu na kuendelea kuwashinikiza katika ujenzi wa maendeleo katika maeneo hayo.

Seneta wa Pokot Magharibi, Profesa John Lonyangapuo na mwenzake wa Turkana John Munyes waliongoza wabunge wakiwemo; Mwakilishi wa wanawake Joyce Emanikor, James Lomenen(Turkana Kusini), Mark Lomunokol(Kacheliba), Samuel Moroto(Kapenguria), Protus Akuja(Loima) na Philip Rotino(Sigor) katika sherehe hizo za kusherekea amani.

Wakati wa mkutano huo viongozi hao walikumbuka zama ambazo hakukuwa na maelewano katika sehemu hizo kutokana na wizi wa mifugo na mapigano ya kikabila.

Aidha viongozi hao walitumia mkutano huo kutoa maombi kwa serikali kuwaajiri vijana wa sehemu hizo, hususan wale waliojinasua kutoka kwa wizi wa mifugo, ambao sasa wanahubiri amani.

Bwana Boinett amewahakikishia viongozi hao kuwa mpango wa kuwaajiri vijana hao umeanza.

Share This
Load More Related Articles
Load More By Reporter
Load More In News

Check Also

​Governor Tolgos working closely with EACC to promote integrity and good governance in Elgeyo Marakwet

Share this on WhatsAppElgeyo Marakwet Governor Alex Tolgos has said he is working closely …